Hafla hiyo imeonesha uzito na heshima kubwa aliyonayo Samahat Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum katika jamii ya Kiislamu na ya kitaifa kwa ujumla.

20 Julai 2025 - 22:06

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Tarehe 20 Julai,  Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mardhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, ameongoza hafla kubwa ya kiheshima katika ukumbi wa DYCC Temeke kwa ajili ya "Walima" wa mwanae Islah, aliyehitimisha Ndoa yake wiki iliyopita nchini Kenya.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Hafla hii imepambwa kwa uwepo wa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Masheikh wakubwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, pamoja na wawakilishi wa dini nyingine, wote wakijumuika kwa utulivu na heshima kubwa kwa ajili kufurahia jambo Tukufu la Ndoa ya Mtoto wa Kiongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mgeni Rasmi wa Hafla hii alikuwa ni: Mheshimiwa Mufti wa Tanzania, Dkt.Abubakar Zubair bin Ally akiambatana na timu kutoka Makao Makuu ya BAKWATA, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, ambao wote kwa pamoja wamehudhuria na kuipamba hafla hii ikiwa ni ishara muhimu ya mshikamano wa kidini na kijamii.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Shekh Muharramu Mwaita alitumia fursa aliyopewa kumpongeza Dkt. Alhad Mussa Salum kwa kuonesha Uongozi bora kwa kuzingatia nyakati za Sala katika ratiba za Hafla mbalimbali, hasa Sala ya Adhuhuri ambayo ilitekelezwa kwa nidhamu Sahihi katika Hafla hiyo, tofauti na baadhi ya hafla nyinginezo ambapo Sala huwa haizingatiwi wakati wake katika ratiba na hivyo kutokupewa kipaumbele kinyume na anavyotaka Mwenyezi Mungu.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Hafla hiyo imeonesha uzito na heshima kubwa aliyonayo Samahat Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum katika jamii ya Kiislamu na ya kitaifa kwa ujumla.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Tukio hili limeacha alama ya mshikamano, heshima na kielelezo cha uongozi wa kiroho wenye maadili.

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Mh.Mufti wa Tanzania,Masheikh mbalimbali, na Viongozi wa Serikali Wajumuika na Sh.Dr.Alhad Mussa Salum katika Hafla ya Kifahari ya Mwanae Islah +Picha

Tumekuwekea hapo chini picha zaidi za tukio hili adhimu

Your Comment

You are replying to: .
captcha